Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Hafla ya kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa kuuawa kishahidi kwa watangulizi wa mhimili wa mapambano, wanazuoni wakubwa wa Kishia na fahari za ulimwengu wa Kiislamu, mashahidi Sayyid Hassan Nasrallah na Sayyid Hashim Safiuddin, imefanyika usiku wa leo Jumatano, 9 Mehr 1404, kwa kuhudhuriwa na wanazuoni maarufu, wahadhiri wa vyuo, taasisi za kimataifa, familia za mashahidi na wananchi wa Qom waliokuwa na mapenzi ya dhati na uongozi, katika ukumbi wa Imam Khomeini (r.a) ndani ya haram tukufu ya Bibi mtukufu Fatimah Masuma (s.a).
Miongoni mwa waliokuwapo ni Ayatollah Muhammad Qomi (Naibu wa Idara ya Mahusiano ya Kimataifa katika Ofisi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi), Ayatollah Reza Ramazani (Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya AhlulBayt a.s), Ayatollah Sayyid Hashim Hosseini Bushehri (Rais wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom), Hujjatul-Islam wal-Muslimin Ali Abbasi (Rais wa Jumuiya ya Al-Mustafa), Hujjatul-Islam wal-Muslimin Hamid Shahriari (Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ukaribu wa Madhehebu ya Kiislamu), pamoja na viongozi wengine, wanafunzi na walimu wa Hawza ya Qom kutoka mataifa mbalimbali, na vilevile wananchi wa Qom na mahujaji wa haram tukufu ya Bibi Fatimah Masuma (s.a).
Sayyid Hassan Nasrallah; mfano kamili wa kutetea wanyonge
Mhubiri mkuu wa hafla hiyo, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Naser Rafi’i, akizungumzia ulinzi wa Waislamu wa Kishia kwa wanyonge alisema: “Imam Hassan Askari (a.s) katika riwaya moja amewataja Mashia kama watu wanaowatanguliza wengine mbele ya nafsi zao. Mateso makubwa aliyoyapata shahidi Sayyid Hassan Nasrallah na wapiganaji wa Hizbullah ya Lebanon yalikuwa kwa ajili ya kuwatetea watu wanyonge wa Gaza. Kutetea wanyonge ni alama ya Shia, kama tulivyojifunza kutoka kwenye madhehebu haya; na tunaposhuhudia tetemeko au mafuriko katika nchi jirani, hatusemi kuwa hayahusiani nasi, bali tunawasaidia wahanga wa maeneo hayo.”
Akieleza sifa za pekee za shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, Rafi’i aliongeza: “Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi katika ujumbe wake wa rambirambi kutokana na kuuawa shahidi kwa kiongozi huyu, alitaja sifa saba muhimu alizokuwa nazo. Yeye (Kiongozi) hutuma ujumbe wake kwa umakini mkubwa. Itakuwa vizuri endapo tafiti za kitaaluma zitatayarishwa kwa ajili ya kuchunguza ujumbe wa rambirambi wa Kiongozi Mkuu, kwani licha ya kutuma salamu za rambirambi kwa watu mbalimbali katika harakati tofauti, sauti na ladha ya ujumbe wake daima hubeba maana tofauti.”
Nafasi ya Shahidi Nasrallah kwa mtazamo wa Kiongozi wa Mapinduzi
Mwalimu wa Hawza ya Qom aliendelea kueleza: Sifa ya kwanza iliyotajwa kwa ajili ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah katika ujumbe wa rambirambi wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ni “Mujahid Mkubwa (مجاهد کبیر)”. Jihadi ni jambo la msingi sana, na shahidi huyu alikuwa ni mujahid mkubwa.
Sifa ya pili iliyotajwa ni kuwa “mbebaji bendera ya mapambano (پرچمدار مقاومت)”. Mapambano ni jambo muhimu, lakini kuwa mbebaji bendera wa mapambano ni muhimu zaidi.
Sifa ya tatu ni kuwa “msomi mwenye heshima na elimu (عالم با فضیلت)”. Shahidi huyu alikuwa mwanachuoni aliyeelimika, na katika ujana wake alikuwa na idhini ya moja kwa moja kutoka kwa Imam Khomeini (r.a) katika mambo mengi.
Rafi’i akiashiria sifa zilizotajwa na Kiongozi wa Mapinduzi kuhusu shahidi Nasrallah alisema: “Kiongozi alisisitiza kuwa Sayyid Hassan Nasrallah alikuwa ‘meneja wa kisiasa’. Wengi ni wanachuoni, lakini siasa hawana; na wengine ni wanasiasa, lakini si wanachuoni. Kuunganisha sifa hizi pamoja katika mtu mmoja ni jambo gumu. Hali hii ilionekana pia kwa Imam Khomeini (r.a) ambaye alikuwa mwanasiasa mahiri, lakini vilevile alikuwa mtu wa Mwenyezi Mungu.”
Akaongeza: “Uongozi wa kipekee (رهبری کمنظیر)” na “meneja na mujahid (مدیر و جهادگر)” ni sifa nyingine zilizotajwa na Kiongozi Mkuu. Aidha, Kiongozi alisema: “Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah hakuwa mtu mmoja tu, bali alikuwa ni shule ya fikra.” Hali hii inakumbusha maneno ya Imam Khomeini (r.a) aliposema kuhusu Shahid Beheshti kwamba: “Yeye ni taifa zima.” Hivyo watu kama hawa walikuwa na upeo mpana zaidi ya zama zao.
Rafi’i alisisitiza: “Bendera ambayo Shahidi Nasrallah aliibeba, haitabaki ardhini. Hakika njia ya mapambano ya Hizbullah ya Lebanon itaendelea. Wengi walijitahidi kuondoa silaha za mapambano, lakini walishindwa. Wakati Yasser Arafat aliposhikana mikono na Wazayuni, watu hawakuamini kwamba miongo michache baadaye, viongozi kama Haniyeh na Sinwar wangekuwa mstari wa mbele wa harakati ya mapambano ya silaha ya Wapalestina dhidi ya Israel.”
Mwalimu huyo wa Hawza Qom akabainisha: “Hizbullah ya Lebanon ni shule ya fikra. Njia ya Shahidi Nasrallah itaendelea. Shahidi huyu alikuwa mtu wa husaynia, wa maombolezo na machozi ya Imam Hussein (a.s). Na leo kaburi lake ni mahali pa kukusanyika wapenda uhuru wa ulimwengu.”
Ahadi ya upinzani kwa damu ya mashahidi
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Mu‘in Daqiq, mwakilishi wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, akizungumza katika tukio hilo aliwasilisha salamu za wananchi wa Lebanon kwa taifa la Iran na kusema: “Ee taifa kuu la Iran, ninawaletea salamu za amiri wa Hizbullah, familia za mashahidi na taifa la Lebanon. Kutoka kando ya haram tukufu ya Bi Fatima Masuma (s.a) nasema kwa Kiongozi wetu: Ewe kiongozi wetu, kama watoto wenu Nasrallah na Safi‘al-Din, tuko mwaminifu kwa ahadi zetu na tunasubiri ishara yenu. Kwa damu ya mashahidi tunafunga ahadi — hata kama shinikizo la maadui litakuwa kubwa, hatutakata tamaa wala kutooa kauli ya ‘هیهات من الذله’ (kamwe hatukubali kunyanyaswa).”
Hatutouacha Uwanja - Hatutawapelekea silaha zetu
Muin Daqiq aliendelea: “Kwa niaba ya mtiririko wa upinzani tunawahakikishia kwamba hatutaondoka uwanjani na hatutawapa silaha zetu. Tutajitahidi kufanya mtaala na njia za mashahidi Nasrallah na Safi‘al-Din zive chombo chetu na ziendelee. Mashahidi hawa hawakuwa watu wa pekee; walikuwa mtaala — na sisi kwa mashahidi hawa tumeahidi kubaki uwanjani na kushikilia bendera ya heshima na utu. Watoto wa mtaala wa Nasrallah na Safi‘al-Din hawana hofu kutokana na shinikizo au vitisho vya adui.”
Mwakilishi wa Hizbullah mjini Qom, akitoa shukrani kwa wale wote waliokuwepo katika hafla ya kumbukumbu ya mashahidi Nasrallah na Safi‘al-Din, alisema pia: “Kwa niaba ya uongozi tunashukuru wale wote waliohudhuria katika hafla hii, na pia tunatambua kwa shukrani Ofisi ya Kiongozi Mkuu na taasisi nyingine zilizounga mkono tukio hili.”
Kutoka kwa ahadi za washiriki hadi Qaswida (Nauha) za sifa bora kwa Ahlul-Bayt (a.s)
Katika sehemu mbalimbali za hafla, wajumbe walihimiza kwa kurusha vitisho dhidi ya ustaarabu wa kibepari na Uzaioni, wakieleza kupinga kwao uhalifu wa utawala wa Kizayuni na wa Marekani katika kuua wananchi wanyonge wa Gaza. Washiriki walifunga ahadi kwa mashahidi wa upinzani kuwa hawataikubali aibu, na wataendeleza njia na maadili ya mashahidi.
Sehemu ya mwisho ya tukio ilijumuisha nyimbo za sifa (madh) kwa Ahlul-Bayt (a.s) zilizotolewa na waimbaji Mas‘ud Zamani na Haj Ali Maleki-Nejad.
Inafaa kutajwa kuwa katika uendeshaji wa hafla hii taasisi na mashirika mbalimbali yalishiriki, yakiwemo:
Ofisi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi katika Qom, Uongozi wa Haram Tukufu ya Bibi Fatimah Masuma (s.a), Jumuiya ya Kimataifa ya Ukaribu wa Madhehebu ya Kiislamu, Jumuiya ya Al-Mustafa al-‘Alamiyyah, Kituo cha Uongozi na Kituo cha Huduma za Hawza, Jumuiya ya Walimu na Baraza Kuu la Hawza, Hawza za wanawake na Jumuiya ya al-Zahra, Ofisi ya Mkoa wa Qom, Shirika la Tablighi la Kiislamu, Ofisi ya Tablighi ya Hawza ya Qom, Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu, vikosi vya kijeshi na vya usalama, Ofisi ya Uwakilishi wa Waliyyul-Faqih katika mambo ya Hija na Ziara, Taasisi ya Aalulbayt, Jumuiya ya Aalulbayt al-‘Alamiyyah, Jumuia ya Imam al-Sadiq (a.s), Jumuiya ya Wawakilishi wa Talaba wa Hawza, pamoja na makundi ya muqawama (Hizbullah, Hashd al-Sha‘abi, Kata’ib, Zaynabiyyun, Fatimiyyun, Haydariyyun, Husayniyyun) na Jumuiya ya Kimataifa ya AhlulBayt (a.s).
Your Comment